Breaking News

Read about Chibu Perfume owned by Diamond Platnum

USIYOJUA KUHUSU PERFUME YA DIAMOND PLATNUMZ.

Mbali na msanii kufanya show,Kupata dili za matangazo na kutegemea mauzo ya Album,lakini bado suala la Ujasiriamali ni muhimu zaidi kwani litamfanya msanii kuendelea kuingiza kipato nje ya kazi zake za kisanii.Mifano ipo mingi sana kwa wasanii wakitaifa na hata wale wakimataifa.

Juzi ilikuwa ni siku nzuri sana kwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz baada ya kutangaza rasmi kuwa na yeye ataingiza manukato (Perfume) yake sokoni very soon!hii ni ishara nzuri ya kuendelea kufanikiwa kwake kwani tayari anamashabiki lukuki sio Tanzania tu bali Afrika na Duniani kote.

Lakini bado kuna maswali chungu nzima juu ya bidhaa hiyo na baadhi ya maswali hayo ni Lini Bidhaa hiyo itatoka rasmi na kuanza kuuzwa madukani?wengine wanauliza itauzwa maduka gani hapa Tanzania?wengine wanataka kujua bei tu ya Perfume hiyo.Sasa DizzimOnline ikaona sio kesi acha ifuatilie kiundani ili iweze kutoa majibu ya maswali ya wadau wetu waliyotuuliza kwani hii itakuwa ni faida kubwa kwa niaba hata ya wale ambao hawajauliza.

Tumemtafuta Meneja wa Diamond Platnumz Sallamkuzungumzia japo kiutandani juu ya “ChibuPerfume” na akajibu maswali yote muhimu juu ya bidhaa hiyo,swali la kwanza lilikuwa ni lini Perfume hiyo itakuwa tayari madukani?

Sallam alisema “Mzigo ‘ChibuPerfume’ upo tayari kinachosubiriwa ni kibali tu,kibali maalum kutoka serikalini kupitia mamlaka yake husika ya TFDA hivyo tukipata kibali mapema hata kabla ya mwaka huu kuisha tutaingiza bidhaa hiyo rasmi sokoni.”

Tulimuuliza tena Perfume hiyo itauzwa kwenye maduka gani? na itapatikana nje ya Nchi?Sallam alisema “Itapatikana kwenye maduka yote makubwa ya bidhaa za urembo hapa Tanzania lakini pia itapatikana karibia nchi zote Afrika kupitia DUTY FREE SHOPS/STORES”

Tuliuliza pia Kuhusu bei ya ‘ChibuPerfume’ alisema “Bei ya chibu perfume bado haijawa rasmi ila wasijali wateja wetu tutawawekea bei ya kawaida itakayoendana na maisha ya kila mtanzania”

Ufafanuzi wa ‘DUTY FREE SHOPS/STORES’ haya ni maduka yasiyotozwa kodi na yanapatikana kwenye viwanja vya ndege vyote Duniani na ndani ya Ndege tu soma zaidi

No comments